Utume Online

 UTUME ONLINE ni huduma ya kichungaji itolewayo na Jumuiya yetu kwa njia ya Internet.

Huduma hii inatolewa kwa lengo la kukusaidai katika safari yako ya imani.  Inatolewa kwa njia mbili:

SWALI: Unalo swali lolote juu ya Imani, Maadili, Kanisa, Biblia au Maisha ya Kiroho kwa ujumla? Andika swali lako katika sehemu wazi hapo chini. Utie pia anuani yako ya Email ili Mchungaji Mhusika aweze kuwasiliana nawe. Kisha bonyeza "Tuma."

OMBI:  Sisi watawa tunasali kila siku kwa ajili ya watu wote. Je, una shida, nia au ombi fulani ambalo ungependa tulijumuishe katika sala zetu za kila siku?  Inaweza kuwa shida binafsi, kumwombe mgonjwa, marehemu, kuomba baraka/mafanikio, n.k. Basi usisite kututumia. Andika ombi, anuani yako ya Email kisha bonyeza "Tuma."

Muhimu: Tungependa kujua Jimbo lako au unawasiliana nasi kutokea wapi. Ni rahisi kwa Mchungaji Mhusika kukusaidia ikiwa utataja hali yako ya maisha kama:  Mwanafunzi, Mtawa, Mwana-Ndoa, Mwanamume/Mwanamke na umri wako. Hata hivyo ujisikie huru. Karibu na Mungu akubariki!