Abasia Yetu Inakua...

KWA KWELI  kila mmoja alighubigwa na tabasalamu la furaha katika sherehe ya Mt. Benedikto mwaka huu. Hii ni kwa sababu siku hiyo jumla ya watawa vijana sita walifunga nadhiri zao - watano nadhiri za muda na mmoja nadhiri za daima. Wanovisi waliofunga nadhiri zao za muda ni Bro Antony (Jimbo la Mbulu), Bro. Bernardo (Dar es Salaam),  Bro. Baltasar (Iringa), Bro. Bonaventura (Tanga) na Bro. Methodius Ssakweli. Huyu anatoka jimbo la Mbulu. Wawili kati ya hawa wameshamaliza masomo yao katika fani za uhasibu na ushonaji. Hawa wataingia kazini moja kwa moja. Wengine wanategemea kusomea masomo ya kipadre, hivyo wataanza masomo ya Falsafa baadaye mwaka huu.

Bro. Revocatus Lilungulu (Jimbo la Lindi) ndiye aliyefunga nadhiri za maisha kwa mwaka huu. Yeye amesomea mambo ya uchapishaji na anafanya kazi katika Idara ya Uchapishaji (Printing Department) ya Ndanda Mission Press. Kitaaluma, pia, ni mwalimu wa maswala ya uchapishaji na lugha kwa vijana wanaojifunza stadi mbalimbali za kazi katika karakana zetu hapa Ndanda. Tunawatakia wote maongozi ya Mungu katika wito na utume wao.

JUU: Bro Revocatus akiwa amejilaza chali wakati wa kuita maombezi ya Watakatifu Wote juu yake.