Tunapopatikana

MAELEZO MUHIMU KUHUSU NDANDA

Tulipo:

Mkoa

Kusini Mashariki mwa  Tanzania

Mtwara 

Wilaya Masasi
Usafiri: Kutoka  Dar es Salaam: Kwa ndege hadi Mtwara, kisha km 160  kwa gari au basi hadi Ndanda. Barabara ni ya lami. Mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Ndanda/Masasi yanapatikana kila siku.  Safari yachukua walau saa 8 hivi.
Hali ya Hewa: Ndanda ni eneo lenye joto hasa miezi ya Septemba hadi Machi. Kuanzia mwezi Mei hadi Julai kuna ubaridi wa kadiri. 
Makabila: Wengi waishio karibu na Ndanda ni Wamakonde, Wamakua na  Wamwera. Idadi ya makabila mengine si kubwa.
Usalama: Usihofu kuhusu usalama wako. Hata hivyo jiangalie wakati utembeapo mwenyewe hasa usiku maeneno tatanishi. Haishauriwi kuogelea kwenye mito. Mamba!
Afya: Ndanda ni eneo lenye mbu wa malaria. Hospitali nzuri yenye dawa na waganga mahiri ipo. Kama si mwenyeji, epuka kunywa maji ya visimani. 
Imani za Kidini:

Wakristu -  ni wengi hasa Wakatoliki na Waanglikana. Pia makanisa mengine madogo kama Wasabato yanapatikana. Walutheri ni wachache. Idadi ya Waislamu ni nzuri.