Mwanzo

Abasia ya Ndanda ni jumuiya ya watawa wanaume wanaoishi kadiri ya kanuni ya Mtakatifu Benedikto.  Lengo letu Mama ni kuishi pamoja tukimfuata Yesu kwa njia ya mapendo ya kindugu, kuhubiri habari njema na kuwatumikia watu wanaotuzunguka. Tungependa kukukaribisha kwa moyo mkunjufu katika Tovuti yetu.

Karibu - Facebook 

Habari

Abasia Yetu Inakua...

SIKUKUU YA MT. BENEDIKTO  iliadhimishwa kwa furaha kubwa hapa Ndanda wakati Vijana wetu wapatao sita walipofunga nadhiri zao.

Idara ya Ujenzi

Ujenzi Ndanda inatambulika kama moja ya vitengo muhimu kabisa katika kazi ya kuinjilisha eneo la Kusini Mashariki mwa Tanzania. Makanisa na majengo mengi mbalimbali yamesanifiwa na kujengwa na idara hii. Pamoja na shuguli za usanifu na ujenzi kwa ujumla, idara ya ujenzi inajihusisha na shuguli za uchongaji wa mawe (sculpturing) kwa lengo la kutengeneza altare, sanamu, viti vya kanisani, n.k.

Mazingira

Utunzaji  Mazingira ni moja ya mambo yapewayo kipaumbele na Watawa wa Ndanda. Katika Jamii ambayo bado si wengi waonao umuhimu wa kutunza mazingira,  abasia ya Ndanda yataka kuonesha umuhimu wa kutunza mazingira. Kwa njia ya upandaji miti na kutunza vyanzo vya Maji, Watawa wa Ndanda wanajaribu kutoa mfano ambao wanatumaini utaigwa na wengine.